
Mkurugenzi wa Mara Online, Jacob Mugini (wakwanza kulia), akikabidhi zawadi ya kompyuta kwa viongozi wa Shule ya Msingi Mary Immaculate Rosana iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara, wakati wa sherehe za mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo juzi.
Tarime
------------
Mkurugenzi wa Mara Online, Jacob Mugini, ametoa zawadi ikiwemo kompyuta (desktop) na fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo cha kisasa katika Shule ya Awali na Msingi Mary Immaculate iliyopo Parokia ya Rosana, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Mugini alikabidhi zawadi hizo juzi Jumanne, Agosti 11, 2026 wakati wa sherehe za mahafali ya saba wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo ambao wanatarajiwa kufanya mtihani wa taifa baadaye mwaka huu.

“Nimefurahi kufika katika shule hii ya Mary Immaculete, pokeeni zawadi yetu kutoka Mara Online kwa ajili ya maendeleo ya taaluma ya shule hii,” Mugini ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara alisema.
Mwanahabari huyo aliwapongeza wanafunzi wanaotarajia kuhitimu elimu ya msingi katika shule hiyo ambayo inasimamiwa na Masista wa Shirika la Jimbo Katoliki Musoma la Moyo Safi wa Maria Afrika (IHSA) na kuwatakia mafanikio katika safari yao ya elimu.
“Nawapongeza kwa hatua mliyofikia, nawapongeza pia wazazi na walimu wenu kwa msaada wanaoendelea kuwapatia ili muweze kufikia ndoto zenu kielimu. Lakini kwa namna ya pekee, nawashukuru walioanzsiha hii shule hapa Rosana,” alisema Mugini ambaye kitaaluma na mwandishi wa habari.

No comments:
Post a Comment