NEWS

Monday, 10 August 2026

Musoma Vijijini: Mwenge wa Uhuru waiagiza TANESCO kuwasha umeme Zahanati ya Kiriba



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda.

Na Mwandishi Wetu
Musoma
-------------

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda, ametoa muda wa siku 21 kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linapeleka umeme katika Zahanati ya Kijiji cha Kiriba kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara.

Mwang'onda alitoa agizo hilo Agosti 8, 2026 baada ya kuarifiwa kuwa ujenzi wa zahanati hiyo umekamilika, vifaa vipo na watumishi wapo, lakini haijaunganishiwa huduma ya umeme.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo na nyumba ya mtumishi yenye thamani ya shilingi milioni 260.5, Mwang’onda aliitaka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kuhakikisha inaanza kutoa huduma kwa wananchi mapema iwezekanavyo.

Akiwa katika mradi huo wa afya, kiongozi huyo wa mbio za mwenge aligawa vyandarua kwa wananchi wa kata ya Kiriba na kuwahamasisha kuvitumia kujikinga dhidi ya malaria.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages