NEWS

Friday, 28 August 2026

Rais Samia ampandisha cheo RC Mara kutoka Kanali kuwa Brigedia Jenerali



Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, akimvisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Alfred Mtambi, cheo cha Brigedia Jenerali, kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan, jijini Dodoma leo Agosti 28, 2028.

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
--------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempandisha cheo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Alfred Mtambi, kutoka Kanali kuwa Brigadia Jenerali, kuanzia Agosti 21, 2026.

Brigedia Jenerali Mtambi na maafisa wengine wa jeshi waliopandishwa vyeo wamevishwa vyeo vyao vipya na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, kwa niaba ya Rais Samia.

Hafla ya kuwavisha vyeo hivyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi jijini Dodoma, leo Ijumaa, Agosti 28, 2026.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages