NEWS

Friday, 28 August 2026

Sagini achomoza uteuzi wa Ma-RC, kuongoza mkoa wa Mbeya



Jumanne Abdallah Sagini

Na Mwandishi Wetu

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Butiama, Naibu Waziri katika wizara za Katiba na Sheria na Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Abdallah Sagini, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mbeya.

Sagini ni miongoni mwa wakuu wa mikoa wapya wanne walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana Alhamisi, Agosti 27, 2026.

Sagini pia amewahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu kabla ya kujitosa kugombea ubunge katika jimbo la Butiama mkoani Mara 2020.

Sagini anaungana na wakuu wa mikoa wengine wapya watatu, Stanslaus Haroon Nyongo (Pwani), Alexander Pastory Mnyeti (Geita) na CP Salum Rashid Hamduni (Mwanza).

Pamoja na uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya, Rais Samia pia amewahamisha wengine kwenda vituo vipya, pamoja na makatibu tawala wa mikoa.

Kupangwa kwa safu za uongozi wa juu wa mikoa lengo lake kubwa ni kuimarisha utendaji wa kazi na kuchochea kasi ya maendeleo ya taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages