
Makamu wa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembe, akizungumza bungeni jijini Dodoma.
Dodoma
--------------
Makamu wa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembe, amesema atakuwa kiongozi wa Watanzania wote bila kubagua mtu yeyote.
"Nitakuwa Makamu wa Rais wa Watanzania wote, sio wa CCM pekee,” Ndejembi amesema katika hotuba yake leo Agosti 28, 2026 jijini Dodoma, mara baada ya Bunge kumthibitisha kuwa Makamu wa Rais.
Ndejembi amethibitishwa kuwa Makamu wa Rais wa 13 Tanzania kwa kupata kura zote 324 zilizopigwa na wabunge, sawa na asilimia 100.
Amewashukuru wabunge kwa kumthibitisha kwa kura zote za kumkubali kushika madaraka hayo.
“Kura mlizonipa mmeonesha kwamba mna imani na Rais na uteuzi alioufanya, na pia mna imani na mimi,” amesema.
Ameahidi kutekeleza majukumu yake kwa unyenyekuvu mkubwa katika kumsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake ya kimaendeleo kwa Watanzania.
"Nitajitahidi sana kwa unyenyekevu mkubwa kumsaidia Mhe. Rais na kuwa kiungo kwa Watanzania wote.
“Ukilipwa kwa utu, lipa kwa utu, ukilipwa kwa wema, lipa wema. Nitakuwa mtiifu kwa Rais na kumsaidia atimize malengo yake kwa Watanzania," amesisitiza Makamu wa Rais Ndejembi.
Ametumia nafasi hiyo pia kuomba ushirikiano wa viongozi katika kuwatumikia Watanzania ili wapate maendeleo wanayoyatarajia kutoka serikalini.
Ndejembi alipendekezwa na kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam juzi, chini ya Mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho tawala, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ndejembi, 43, ambaye alikuwa Waziri wa Nishati, anamrithi Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyejiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais, Agosti 25, 2026.
No comments:
Post a Comment