
Mkazi wa mtaa wa Bomani mjini Tarime mkoani Mara, akifurahia huduma ya maji safi ya bomba nyumbani kwake kama alivyokutwa na camera ya Mara Online News, jana Jumatano.
Tarime
------------
Wakazi wa mtaa wa Bomani mjini Tarime wanaendelea kupata maji safi ya bomba baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) kuzibua bomba lililokuwa limeziba na kusababisha baadhi ya wateja kukosa huduma hiyo kwa siku kadhaa.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na MUWASA, matengenezo hayo ambayo yalifanyika Agosti 18, 2026 pia yalisababisha maji kuchanganyikana na tope ambalo lilibadilisha uhalisia wa rangi ya maji katika eneo hilo,
Hata hivyo, kumekuwa na picha mjongeo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha maji yakitoka kwenye bomba yakiwa na rangi isiyokuwa ya kawaida hata baada ya huduma ya maji safi kurejea.
Habari njema ni kwamba wakazi wa mtaa wa Bomani walizungumza na Mara Online News jana Jumatano na kuthibitisha kuwa kwa sasa mabomba yanatoa maji safi na wanaendelea kupata huduma hiyo kama kawaida.
Aidha, wataalamu wa MUWASA) walifika katika mtaa wa Bomani jana Jumatano na kufanya ufuatiliaji wa hali halisi ya huduma ya maji ya bomba.

Katika ziara hiyo, wataalamu wa MUWASA walishuhudia na kujiridhisha kuwa wakazi wa mtaa huo wanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama ya bomba kama kawaida.
"Mimi kwangu ninapata maji masafi, machafu sijayaona. Kama kuna mtu kwake maji yanatoka machafu, afuatilie vizuri, labda laini yake imetoboka,” alisema mkazi wa mtaa wa Bomani aliyejitambulisha kwa jina la Mama Monica.
Mama Monica
Mama MonicaMkazi mwingine wa mtaa huo, Ester Athanas Pascal, naye alithibitisha upatikanai wa huduma ya maji safi ya bomba nyumbani kwake. "Sioni changamoto yoyote hapa kwangu, ukifungulia bomba maji yapo, sioni shida,” alisema.
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Andieli, alisema: "Kwangu sioni tatizo kwenye maji, yanapatikana na ni masafi.”
Naye Kambarage Mantago, alisema: "Hapa Bomani mimi naona maji yako sawa, kwangu ninapata maji saa zote mpaka chooni, na ninalipa bili yangu kwa wakati.”
Kambarage Mantago
Kambarage MantagoUshuhuda huo wa wakazi wa mtaa wa Bomani umeonesha hali tofauti na taswira iliyojengwa na taarifa iliyosambazwa mitandaoni.
Mbali na mji wa Tarime, MUWASA pia inasambaza huduma ya majisafi kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, miji ya Shirati wilayani Rorya na Mugumu wilayani Serengeti.
Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa MUWASA imefanikiwa kuvuka lengo la Ilani ya CCM la kufikia asilimia 95 ya wananchi wanaopata maji safi mijini kufikia mwaka 2025, huku ikifikia asilimia 98 ya wanaopata huduma hiyo katika Manispaa ya Musoma.
No comments:
Post a Comment