NEWS

Sunday, 30 August 2026

Wamiliki wa miradi ya uchimbaji mdogo wa madini wapewa siku 30 kurekebisha kasoro




Na Mwandishi Wetu
Dodoma
--------------

Wamiliki na wawezeshaji wa miradi ya uchimbaji mdogo wa madini yenye mikataba ya msaada wa kiufundi wamepewa siku 30 za kurekebisha upungufu uliobainika wakati wa ukaguzi.

Agizo hilo lilitolewa na Tume ya Madini hivi karibuni jijini Dodoma baada ya kubainika kwa kasoro za utekelezaji kupitia ukaguzi.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Ramadhani Lwamo, alionya kuwa watakaoshindwa kurekebisha upungufu huo katika kipindi kilichotajwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Lwamo alisema hatua hizo ni pamoja na kufutiwa ridhaa ya msaada wa kiufundi.

Alieleza kwamba agizo la kurekebisha upungufu uliobainika kwenye miradi ya uchimbaji linafuatia ukaguzi wa miradi 128.

Kati ya miradi hiyo, 42 ilibainika kutofanya kazi, 86 inaendelea na shughuli zake huku ikikabiliwa na changamoto za utekelezaji na uzingatiaji wa masharti ya mikataba ya msaada wa kiufundi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages