
Simba ndani ya NCAA
Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) mkoani Arusha imesema simba 10 wameuawa katika eneo la Ndutu, kata ya Endulen.
NCAA ilieleza katika taarifa yake kwa umma jana Jumamosi kwamba imebaini kuwa wanyamapori hao waliuawa Septemba 18, 2026.
“Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa wanyama hao wanaweza kuwa waliuawa kwa kulishwa sumu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Tayari mamlaka imeanzisha uchunguzi wa kina wa kitaalamu ili kubaini chanzo na watu waliohusika katika tukio hilo.
Simba ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii vinavyotajwa kuitangaza NCAA kimataifa.
No comments:
Post a Comment