
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi (aliyevaa suti nyeusi), katika picha ya pamoja na wanafunzi na wahadhiri wa OUT Mara, ofisini kwake mjini Musoma wiki iliyopita wakati wa hafla ya kuwaaga kwenda Ujerumani kwa ziara ya mafunzo.
Musoma
--------------
Wanafunzi 10 na wahadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Tawi la Mkoa wa Mara, wataondoka nchini kwenda Ujerumani kwa mafunzo ya muda mfupi.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ilisema lengo ni kupata mafunzo na kubadilishana uzoefu katika masuala ya Elimu Jumuishi katika Chuo Kikuu cha Ludwig Maximilian cha Ujerumani.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanafunzi na wahadhiri wao wanategemea kushiriki katika awamu ya tatu ya programu hiyo inayotekelezwa kati ya OUT na Chuo Kikuu cha Ludwig Maximilian kilichopo katika mji wa Munich.

Wasomi hao waliagwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi, katika hafla fupi iliyofanyika wiki iliyopita.
Brigedia Jenerali Mtambi aliwataka wanafunzi hao kutumia vizuri fursa hiyo kujifunza ili watakaporudi nchini waboreshe utendaji kazi na kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.


Ludwig Maximilian University of Munich
Chanzo cha habari hii ni Gazeti la Sauti ya Mara
No comments:
Post a Comment