NEWS

Friday, 4 September 2026

Waziri Mavunde aongoza kikao cha Barrick na wachimbaji wadogo wa madini



Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (kulia), akiongoza kikao cha utatuzi wa mgogoro wa haki madini na haki ardhi baina ya kampuni ya Barrick na wachimbaji wadogo wa madini wa wilayani Tarime, kilichofanyika jijini Dodoma leo Septemba 4, 2026.

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
--------------

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameongoza kikao cha utatuzi wa mgogoro wa haki madini na haki ardhi baina ya kampuni ya Barrick na wachimbaji wadogo wa madini wa wilayani Tarime, mkoani Mara.

Kikao hicho cha maridhiano, kimefanyika leo Ijumaa, Septemba 4, 2026 jijini Dodoma, ambapo Waziri Mavunde amezitaka pande zote mbili kukaa na kujadiliana ili kuangalia namna ya bora ya kufikia muafaka kwa kuzingatia maelekezo ya Sheria ya Madini Sura 123.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya Tarime, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Katibu Mtendaji Tume ya Madini, Katibu Tawala Wilaya ya Tarime, Wawakilishi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara na walalamikaji.

Mgodi huo ambao upo wilayani Tarime, unaendeshwa na Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Waziri Mavunde akizungumza katika kikao hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward na Gowele.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages