
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya, akikabidhi zawadi mbalimbali jana Jumamosi kwa walimu wa shule za jimbo hilo zilizofanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne mwaka jana.
Bunda
------------
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya, ametoa na kukabidhi zawadi za fedha taslimu, tuzo na vyeti vya pongezi kwa shule za msingi tano na sekondari tano za jimbo hilo zilizofanya vizuri katika mitihani ya taifa ya darasa la saba na kidato cha nne mwaka jana.
Aidha, walimu 16 waliofaulisha vizuri wanafunzi katika masomo yao, Idara ya Elimu Awali na Msingi, na Idara ya Elimu Sekondari nao wamepewa zawadi za fedha taslimu na vyeti vya pongezi.
Bulaya alikabidhi zawadi hizo zenye thamani ya shilingi milioni 17 wakati wa Tamasha la Walimu lililofanyika Oktoba 24, 2026 katika viwanja vya Shule ya Msingi Bunda.
Kila shule iliyofanya vizuri ilizawadiwa shilingi 1,000,000 na tuzo, huku kila mwalimu aliyefaulisha vizuri wakipewa shilingi 200,000 na cheti cha pongezi.
Mbunge huyo alitoa zawadi hizo kuonesha kutambua na kuthamini mchango wa walimu katika kuinua kiwango cha elimu, kuhamasisha uwajibikaji na ushindani chanya wa shule na walimu.
Aliwapongeza walimu na shule zilizofanya vizuri katika mitihani hiyo, akisema juhudi zao ni msingi wa mafanikio ya wanafunzi na maendeleo ya jamii.
Alisema walimu wana nafasi muhimu katika kujenga msingi wa maarifa, ujuzi na maadili kwa wanafunzi, hivyo ni muhimu kuthamini kazi yao na kuwatia moyo wa kuendelee kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kujituma.
No comments:
Post a Comment