
Harry Kane kulia na Alexia Putellas kushoto wakifurahia ushindi wao wa Tuzo za Balloon d'Or 2026
Mshambuliaji wa Bayern Munich ya Ujerumani na Nahodha wa Timu ya Taifa ya England, Harry Kane, ametwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kiume wa Mwaka 'Ballon d’Or' 2026 katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo jijini London, Uingereza.
"Wow wow wow!" alisema Harry Kane alipopanda jukwaani kupokea tuzo yake.
"Karibu niishiwe maneno. Kuwa hapa London kumefanya usiku huu kuwa wa kipekee zaidi kwangu. Imekuwa bahati nzuri usiku wa leo. Asanteni wote mlionipigia kura. Ninaweza kufikiria haikuwa rahisi kufanya uamuzi mwaka huu.
“Kuna wachezaji wengi wa kiwango cha dunia waliopo hapa usiku wa leo. Hongereni washindi wote na walioteuliwa,” Alisema Kane na kuendelea:
“Mmeonesha kwa namna ya kuvutia kwamba dhamira, kujituma na jitihada vinaweza kuleta mafanikio makubwa."

Harry Kane akifurahia ushindi wa Tuzo ya Ballon d'Or 2026
Kane, mwenye umri wa miaka 33, amefanikiwa kushinda tuzo hiyo akiwapiku washindani wake wa karibu, Kylian Mbape aliyeshika nafasi ya pili na Lamine Yamal aliyeshika nafasi ya tatu.
Ushindi huo unamfanya Kane kuwa Mwingereza wa kwanza kutwaa Tuzo ya Ballon d’Or tangu Michael Owen alipoitwaa mwaka 2001.
Mbali na tuzo hiyo, Kane pia alishinda Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka 'Gerd Müller Trophy" baada ya kufunga magoli 73 katika michezo 65 ya klabu na timu ya taifa katika msimu wa 2025/26.
Kwa upande wa wanawake "Ballon d'Or Feminin" mchezaji wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Alexia Putellas, aliibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa mara ya tatu.

Alexia Putellas akifurahia ushindi wa Tuzo ya Ballon d'Or 2026
Tuzo za Ballon d'Or hutolewa kila mwaka na jarida la France Football kwa wanasoka waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment