
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Pili uliofanyika kimkoa mjini Musoma leo Oktoba 22, 2026.
Musoma
----------------
Kaya 21,279 zenye jumla ya watu 44,786 mkoani Mara zinatarajiwa kusajiliwa kwenye Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Pili.
Msambichaka akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo
Msambichaka amesema uzinduzi huo unalenga kuendelea kutambua, kusajili na kugawa kadi za bima ya afya kwa ajili ya huduma za matibabu kwa walengwa, zikiwemo kaya zenye uhitaji, makundi maalum na jamii kwa ujumla.
Mkuu wa Mkuoa akigawa kadi za Bima ya Afya kwa wananchi wakati wa uzinduzi huo
Brigedia Jenerali Mtambi ametumia nafasi hiyo pia kuwataka wakuu wa wilaya kushirikiana na halmashauri kuhakikisha wananchi wote waliobaki wakati wa Awamu ya Kwanza wanasajiliwa kwenye mpango huo.

Sehemu ya viongozi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo, akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Mara, Ayub Mwita Makuruma (kulia).
"Niwaagize wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha wanakwenda kutekeleza mpango huu nyumba kwa nyumba, kuweka mazingira rafiki kwa wananchi kupata taarifa sahihi na uwepo wa vituo vya kutosha vya kusajili walengwa.
Brigedia Jenerali Mtambi akimsalimia mwananchi mwenye ulemavu aliyehudhuria hafla ya uzinduzi huo.
Aidha, ametaja faida za mpango huo wa Bima ya Afya kwa Wote kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi, uhakika wa kupata matibabu katika ngazi zote na kupanua wigo wa wananchi kupata huduma bora za matibabu bila kujali hali zetu za kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Mtambi na wananchi wakifurahia kucheza wakati wa hafla ya uzinduzi huo wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote. (Picha zote na Mara Online News)




No comments:
Post a Comment