
Mfanyabiashara Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) na wasaidizi wake wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Oktoba 21, 2026 muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ziara ya kibiashara ya siku tano.
Dar es Salaam
--------------------
Mfanyabiashara wa Tanzania, mtunzi na mchapishaji mashuhuri wa vitabu, Nyambari Nyangwine, leo Jumatano Oktoba 21, 2026 ameondoka nchini kwenda nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ziara ya siku tano ya kibiabishara na uwekezaji.
“Nimepata mwaliko maalum wa kufanya ziara ya siku tano katika nchi za UAE za Dubai, Abu Dhabi na Sharja kwa ajili ya shughuli za biashara na ushirikiano katika uwekezaji,” amesema.
Nyambari ambaye ni Mwenyekiti wa Nyambari Nyangwine Group of Companies Limited (NNGCL), alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuanza safari yake.
Mfanyabiashara huyo anafanya ziara hiyo siku chache baada ya kuandaa Kongamano la Kimataifa la Biashara na Uwekezaji jijini Dar es Salama, ambalo lilihudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali, zikiwemo nchi za UAE.
“Katika ziara yangu hii tutajadiliana na wenzetu kwenye maeneo ambayo wanaweza kufanya uwekezaji hapa Tanzania,” amesema Nyambari.
No comments:
Post a Comment