NEWS

Thursday, 5 November 2026

BoT yawaongezea watumiaji wa huduma za kifedha njia rahisi ya kuwasilisha malalamiko



Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
--------------------

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewaongozea watumiaji wa huduma za kifedha fursa ya kuwasilisha malalamiko na kufuatilia utatuzi wake kwa urahisi kupitia mfumo wa kidijitali wa Sema na BoT.

Hatua inalenga kuimarisha ulinzi wa watumiaji wa huduma za kifedha nchini na kuwapa nafasi ya kudai haki zao wanapokabiliana na changamoto.

Vilevile, mfumo huo unalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za malalamiko, kuongeza uwazi na ufanisi katika kushughulikia changamoto zinazotokana na huduma za kifedha zinazotolewa na benki na taasisi nyingine za fedha.

Afisa Benki Kuu kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Janeth Kiwia, amesema mfumo huo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha watumiaji wa huduma za kifedha wanalindwa na wanapata haki zao wanapokumbana na huduma zisizoridhisha.

Afisa Benki Kuu Janeth Kiwia

Kiwia alikuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo Alhamisi, Novemba 5, 2026 wakati wa semina ya siku tatu iliyoandaliwa na BoT kwa waandishi wa habari za uchumi na masoko ya fedha nchini.

Amesema BoT ina jukumu la kusimamia taasisi za fedha zinavyopokea, kushughulikia na kutatua malalamiko ya wateja, ili kuhakikisha hakuna mtumiaji anayekosa haki yake kutokana na kukosa njia ya kufikisha changamoto anazokutana nazo.

Kwa mujibu wa Kiwia, usimamizi huo unazingatia sheria na miongozo ya mwaka 2019 na 2025 inayozitaka taasisi za fedha kuwa na mifumo mizuri ya kupokea na kutatua malalamiko kwa njia mbalimbali, ikiwemo simu, barua pepe, barua za kawaida na madawati ya huduma kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages