
Mgeni rasmi, Mthibiti Ubora wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Abas Munde, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wakati wa Mahafali ya Tisa ya Shule ya Sekondari Tarime Mchanganyiko, Novemba 1, 2026. Kushoto ni Mkurugenzi wa PMF, Hezbon Peter Mwera.
Shule ya Sekondari Tarime Mchanganyiko inayomilikiwa na Taasisi ya Professor Mwera (PMF) chini ya Mkurugenzi wake, Hezbon Peter Mwera, jana Jumapili, Novemba 1, 2026 ilisherehekea Mahafali ya Tisa ya Wahitimu wa Kidato cha Nne.
Mgeni rasmi, Abas Munda (wa pili kulia waliokaa), Mkurugenzi wa PMF, Hezbon Peter Mwera (wa pili kushoto), Mkuu wa Shule ya Sekondari Tarime Mchanganyiko, Mwl. Mwita Samson Marwa (kulia) na wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi, Abas Munde, akikabidhi cheti cha pongezi kwa mzazi bora katika ufuatiliaji wa maendeleo ya taaluma na mienendo ya mtoto wake akiwa shuleni.
Mgeni rasmi na viongozi wengine, walimu na wazazi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mahafali hayo

Wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Tarime Mchanganyiko wakiwa kwenye sherehe ya mahafali yao.

Wahitimu wa kidato cha nne wakiimba na kucheza kwa madaha wakati wa mahafali yao. (Picha zote na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment