
Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Saidi Ally Mohamed, akitangaza Matokeo ya Darsa la Saba.
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2026.
Watahiniwa 970,876 wa mtihani huo wamefaulu kwa madaraja ya A, B na C, sawa na asilimia 85.22 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumanne, Novemba 3, 2026, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Saidi Ally Mohamed, amesema watahiniwa 1,139,273 walifanya mtihani huo.
Katika hatua nyingine, Prof. Saidi amesema watahiniwa 31 wamefutiwa matokeo kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani.
Amefafanua kuwa kati ya watahiniwa hao, 26 wamefutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu, huku watano wakichukuliwa hatua kutokana na kuandika matusi kwenye karatasi za majibu.
BONYEZA HAPA KUTAZAMA MATOKEO >> MATOKEO YA DARASA LA SABA 2026
No comments:
Post a Comment