NEWS

Wednesday 24 July 2019

SERIKALI YA KENYA YAKABIDHI KILO 35.34 ZA MADINI YA DHAHABU ILIYOKAMATWA IKITOROSHWA KWA SERIKALI YA TANZANIA, RAIS MAGUFULI AMPIGIA RAIS KENYATTA KUMSHUKURU LIVE


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi kulia akipokea shehena ya dhahabu kutoka kwa Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Dk. Monica Juma, Ikulu leo Julai 24, 2019.

Na Mwandishi wetu
Serikali ya Kenya leo Julai 24 2019  imekabidhi kwa serikali ya Tanzania dhahabu yenye uzito wa kilo 35 iliyokamatwa na maafisa wa usalama  katika Uwanja wa ndege  wa kimataifa wa Jomo Kenyatta  mwezi wa pili mwaka jana.

Serikali ya Kenya pia imekabidhi  kwa Serikali  ya Tanzania mamilioni  ya fedha ambayo yalikamatwa  nchini Kenya mwaka 2004.

Rais John Magufuli ameshuhudia makabidhiano  hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam  na Kuhudhuriwa pia na Makamu Wa Rais Mama Samia  Suhulu Hassan pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya.

Ujumbe wa Rais Kenyatta kutoka Kenya uliwasilishwa  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Dr. Monica Juma.
Rais Magufuli amemshukuru Rais Kenyatta  kitendo hicho ambacho amesema kinaonesha upendo wa hali ya juu .
“ Namshukuru sana  sana rafiki yangu Uhuru Kenyatta kwa Upendo na Uaminifu  wake”, amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli pia amempigia Rais Kenyatta simu na kuongea naye live kumshukuru ambapo viongozi hao wawili   wameapa kuhakikisha rasilimali  zilizopo  Tanzania na Kenya zinasadia kubadilisha maisha ya wananchi na sio vinginevyo.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages