Na Mwandishi wetu
Serikali ya Kenya leo Julai 24 2019 imekabidhi kwa serikali ya Tanzania dhahabu
yenye uzito wa kilo 35 iliyokamatwa na maafisa wa usalama katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwezi wa pili mwaka jana.
Serikali ya Kenya pia imekabidhi kwa Serikali
ya Tanzania mamilioni ya fedha
ambayo yalikamatwa nchini Kenya mwaka
2004.
Rais John Magufuli ameshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam
na Kuhudhuriwa pia na Makamu Wa Rais
Mama Samia Suhulu Hassan pamoja na
viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya.
Ujumbe wa Rais Kenyatta kutoka Kenya uliwasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Dr. Monica Juma.
Rais Magufuli amemshukuru Rais Kenyatta kitendo hicho ambacho amesema kinaonesha
upendo wa hali ya juu .
“ Namshukuru sana
sana rafiki yangu Uhuru Kenyatta kwa Upendo na Uaminifu wake”, amesema Rais Magufuli
Rais Magufuli pia amempigia Rais Kenyatta simu na
kuongea naye live kumshukuru ambapo viongozi hao wawili wameapa kuhakikisha rasilimali zilizopo Tanzania na Kenya zinasadia kubadilisha maisha
ya wananchi na sio vinginevyo.
No comments:
Post a Comment