Na mwandishi wetu
Rais John Magufuli ameawapisha viongozi walioteuliwa jana baada ya kufanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri.
Walioapishwa leo
saa tatu asubuhi ni Waziri mpya wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais(Muungano na Mazingira), George
Simbachawene na Naibu Waziri mpya
wa Kilimo Hussein Bashe.
Simbachawene amechukua nafasi ya January Makamba
ambaye uteuzi wake ulitengulia na Rais
Magufuli jana huku Bashe akichukua
nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na
Biashara hivi karibuni.
Rais Magufuli amewataka kutekeleza majukumu yao vizuri ili kukidhi matarajio
ya watazania.
No comments:
Post a Comment