Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) leo Disemba 19, imesema kilichokea katika kijiji chha Tatwe Wilayani Rorya hivi karibuni sio mlipuko wa Volkano.
Mtendaji Mkuu wa GST Dr Musa Budeba ametoa taarifa
hiyo kwa vyombo vya habari leo wakati
alipopata nafasi ya kuongea katika mkutano wa mkuu wa klabu ya waandishi wa
habari Mkoa wa Mara(MRPC) .
Dr Budeba amesema walipopata taarifa hizo
walilazimika kusafiri haraka kuelekea katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi
wa awali ambao umeonesha kilichotekea
sio volkano.
“ Kilichotekea sio Volkano bali ni maji yalizidi
udongo na hivyo kusababisha udongo
kuporomoroka( landslide”, amesema Dr Budeba.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo amewataka waandishi wa habari kuwa makini wakati wanapokuwa wanaripoti kuhusu masuala ambayo yanaweza kusababisha hofu au taharuki katika jamii.

sawa kaz nzur
ReplyDelete