NEWS

Thursday 19 December 2019

KILICHOTOKEA RORYA SIO VOLKANO




Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) leo Disemba 19, imesema  kilichokea katika kijiji chha Tatwe Wilayani Rorya hivi karibuni  sio mlipuko wa Volkano.
Mtendaji Mkuu wa GST Dr Musa Budeba ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari  leo wakati alipopata nafasi ya kuongea katika mkutano wa mkuu wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Mara(MRPC) .
Dr Budeba amesema walipopata taarifa hizo walilazimika kusafiri haraka kuelekea katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa awali ambao umeonesha  kilichotekea sio volkano.
“ Kilichotekea sio Volkano bali ni maji yalizidi udongo  na hivyo kusababisha udongo kuporomoroka( landslide”, amesema Dr Budeba.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika  mkutano huo amewataka waandishi wa habari kuwa makini wakati wanapokuwa wanaripoti kuhusu masuala ambayo yanaweza kusababisha hofu au taharuki katika jamii.

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages