WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Kassim Majaliwa jana Machi 21, 2020 alionya upotoshaji na utoaji
holela wa taarifa za ugonjwa wa Corona unaofanywa na baadhi ya watu nchini.
Kufutia hali hiyo, Majaliwa
ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufuatilia watu wanaofanya
vitendo hivyo kupitia mitandao ya kijamii ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Ameagiza kuanzia sasa taarifa
zinazohusu Corona zitatolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto na ikilazimika zitatolewa na Waziri Mkuu, ikilazimika sana
zitatolewa na viongozi wakuu wa nchi ili kuepusha mikanganyiko.
No comments:
Post a Comment