NEWS

Sunday 22 March 2020

Waziri Mkuu Tanzania aonya upotoshaji taarifa za Corona


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa jana Machi 21, 2020 alionya upotoshaji na utoaji holela wa taarifa za ugonjwa wa Corona unaofanywa na baadhi ya watu nchini.

Kufutia hali hiyo, Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufuatilia watu wanaofanya vitendo hivyo kupitia mitandao ya kijamii ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Ameagiza kuanzia sasa taarifa zinazohusu Corona zitatolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na ikilazimika zitatolewa na Waziri Mkuu, ikilazimika sana zitatolewa na viongozi wakuu wa nchi ili kuepusha mikanganyiko.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages