NEWS

Tuesday 28 April 2020

BARIADI YAPOKEA MASHINE 4 ZA KUPUMULIA NA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 5.1 KUJINGGA NA CORONA

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akionesha fedha zilizotolewa na wadau wa maendeleo kwaajili ya kununua vifaa vya kujikinga na maambukuzi ya virusi vya corona wilayani hapo.

Mkuu wa  wilaya  ya Bariadi Festo Kiswaga amepokea msaada wa mashine nne (4) za kupumulia kutoka kituo cha afya Songambele kinachomilikiwa na mtu binafsi ikiwa ni mwendelezo wa wilaya kujiweka tayari kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Mbali na mchango huo pia amepokea kiasi cha shilingi milioni 5.1 kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani hapo ambazo zitasaidia ununuzi wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine hizo kwa mkuu wa wilaya hiyo mganga mkuu wa kituo cha afya cha Songambele kilichopo katika kata ya Nkololo wilayani hapo Dkt. Hellena Sindano amesema  wameamua kutoa mashine hizo kwa matumizi ya muda katika kipindi hiki cha maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona .

Aidha Dkt. Sindano ameongeza kuwa  tayari kituoni  wameweka kifaa maalum cha kisasa kinachoweza kupima joto la mwili  pasipo kumgusa wala kumsogelea mtu.

"katika kipindi hiki cha maambukizi  ya ugonjwa wa corona kituo cha afya cha Songambele tumeamua kutoa mashine 4 za kupumulia ambazo zitamsaidia mtu mwenye shida ya upumuaji na  lengo ni kukabiliana na ueneaji wa maambukizi ugonjwa huu" Alisema Dkt Sindano

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akimkabidhi  mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya mji wa Bariadi  fedha zilizotolewa na wadau wa maendeleo kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya kukabiliana na maambukuzi ya virusi vya corona wilayani hapo.
Nao waganga wakuu akiwemo Dkt. Judith Ringia wa halmashauri ya mji wa Bariadi na  Dkt. Joseph Mziba kutoka wilaya ya Bariadi  wamewashukuru wadau hao huku wakitoa rai kwa wadau hao na wengine  zoezi hilo lisiishie siku moja na  badala yake  liwe zoezi endelevu mpaka ugonjwa utakapoisha .

Kwa upande wao wadau wamesema  wameamua kuunga jitihada za serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa  Tanzania kwani ugonjwa huo unagusa jamii nzima ya Watanzania na dunia  kwa ujumla. 

(Habari na Anita Balingilaki, Bariadi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages