New Zealand imeingia katika hatua mpya katika amri kali iliyokuwa imeiweka wakati huu wa janga la virusi vya corona Jumatatu ambapo baadhi ya shule na biashara zimefunguliwa tena.
Serikali imeripoti leo maambukizi matano mapya tu na Waziri Mkuu Jacinda Ardern amesema mamlaka husika zitaendelea kufuatilia maambukizi yoyote yale mapya. New Zealand inamaambukizi 1,100 yaliyothibitishwa kwa vipimo na vifo 19.
“Hakuna maambukizi yalioenea, na kushindwa kutambuliwa katika jamii nchini New Zealand,” Ardern ametangaza. “Tumeshinda vita hiyo.”
Kulegezwa kwa masharti hayo kutaruhusu watu 400,000 kurejea makazini.
Ni kipindi cha mwezi mmoja tangu New Zealand ilipowataka watu kutotoka majumbani na kuamuru shughuli zote ambazo siyo muhimu kufungwa.
Ardern amesema ni mapema mno kusema lini nchi hiyo itafikia kuwa haina maambukizi ya COVID-19, hatua ambayo ni muhimu kuweza kufunguwa tena kikamilifu shughuli zote nchini.
VOA Swahili.
VOA Swahili.
No comments:
Post a Comment