NEWS

Tuesday 28 April 2020

DC afunga mgodi ulioua mifugo Tarime


Mkuu wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Mhandisi Mtemi Msafiri(wakwanza kushoto), amefunga mgodi unaomilikiwa na mchimbaji mdogo katika eneo la Nyamongo, baada ya kutiririsha maji yanayohofiwa kuwa na kemikali za sumu na kuua ng’ombe 34 na kondoo mmoja waliokunywa maji hayo.

Mhandisi Msafiri ametoa maagizo hayo baada ya kuzuru katika mgodi huo uliopo kijiji cha Kewanja jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, jana Jumatatu jioni saa kadhaa baada ya tukio hilo.

Mkuu huyo wa wilaya ameshuhudia mizoga ya ng’ombe waliokufa baada ya kunywa maji hayo yaliyotiririka kutoka kwenye shimo la kusafisha mchanga wenye dhahabu mgodi huo.
 
Shimo la kusafisisha mchanga wenye dhahabu lililotiririsha maji yalioua ng’ombe na kondoo
Aidha, Msafiri ameagiza wataalamu wa mazingiira kuzungukia migodi yote ya wachimbaji wadogo kukagua kama inazingatia usalama wa mazingira na viumbe hai.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja, Bunini John, amesema ng’ombe waliokufa ni mali ya familia mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages