NEWS

Saturday 18 April 2020

Dkt Chacha ampongeza JPM vita ya COVID-19


DAKTARI Msaidizi wa binadamu, Dishon Chacha, amempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa juhudi zake za kuhimiza wananchi kufanya maombi na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababisha homa kali ya mapafu.

“Rais Dkt Magufuli kwa kweli amekuwa rais wa pekee, amekuwa mstari wa mbele kusisitiza watu wafanye maombi kwa Mungu na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya kujikinga na maambukizi ya COVID-19.

Akizungumzia huduma za afya, Dkt Chacha ambaye ni mtumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana – Butimba jijini Mwanza ameiomba serikali kuimarisha upatikanaji wa vifaa kinga vyenye viwango vya ubora unaotakiwa kwa watumishi wa sekta hiyo kwa ajili ya kujikinga na kuwahudumia kikamilifu washukiwa wa ugonjwa huo.

Aidha, Daktari huyo ametumia nafasi ya mazungumzo na Mara Online News leo Aprili 18, 2020 pia kusisitiza maelekezo ya wataalamu wa afya na serikali ya kuwataka wananchi kuzingatia njia za kujikinga na COVID-19 ikiwemo kunawa mikono kwa vitakasa mikono na maji tiriri na kuepuka misongamano.

(Habari na Christopher Gamaina, Mwanza)No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages