NEWS

Monday 13 April 2020

Kata yajenga secondary ya pili Musoma VijijiniWAKAZI wa kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) katika jimbo la Musoma Vijijini, Mara wameamua kujenga sekondari ya pili kuwapunguzia wanafunzi mrundikano madarasani.
 Shule mpya ya Sekondai ya Seka pia itawapunguzia wananfunzi umbali wa kutembea kutoka vijiji vya Seka, Mikuyu na Chumwi kwenda kusoma katika sekondari ya kata.
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyamrandirira, Muswaga Itra amesema wakazi wa vijiji vyote vitano wanachangia nguvu kazi na fedha taslimu ili kufanikisha ujenzi wa sekondari hiyo.
 Itra ameongeza kuwa Mgodi wa Dhahabu wa Seka umechangia ujenzi huo tripu 23 za mawe na moja ya mchanga, huku Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo akichangia saruji mifuko 250.
 Diwani wa Kata hiyo, Obadia Maregesi amesema ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na miundombinu mingine muhimu itakamilika kabla ya Septemba 2020.
Mbunge wa jimbo, Profesa Muhongo ametoa wito kwa wazawa wa kata ya Nyamrandirira wanaoishi nje ya kata hiyo kujitokeza kuchangia ujenzi wa shule hiyo.

(Habari na Hamisa Gamba, Msaidizi wa Mbunge)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages