NEWS

Monday 13 April 2020

Wagonjwa wapya 14 wa COVID-19 waongezeka Tanzania


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo Jumatatu Aprili 13, 2020 ametoa taarifa ya kuongezeka kwa wagonjwa wapya 14 wa COVID-19 Tanzania na kufanya idadi ya walioambukizwa maradhi hayo nchini kufikia 46 kutoka 32 waliotolewa taarifa Aprili 10, 2020.

Waziri Mwalimu amesema wagonjwa hao wapya wote ni Watanzania, 13 wapo jijini Dar es Salaam na mmoja jijini Arusha na wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages