WAKAZI
wa kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na
Seka) katika jimbo la Musoma Vijijini, Mara wameamua kujenga sekondari ya pili
kuwapunguzia wanafunzi mrundikano madarasani.
Shule
mpya ya Sekondai ya Seka pia itawapunguzia wananfunzi umbali wa kutembea kutoka
vijiji vya Seka, Mikuyu na Chumwi kwenda kusoma katika sekondari ya kata.
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Nyamrandirira, Muswaga Itra amesema wakazi wa vijiji vyote
vitano wanachangia nguvu kazi na fedha taslimu ili kufanikisha ujenzi wa
sekondari hiyo.
Itra
ameongeza kuwa Mgodi wa Dhahabu wa Seka umechangia ujenzi huo tripu 23 za mawe
na moja ya mchanga, huku Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo
akichangia saruji mifuko 250.
Diwani
wa Kata hiyo, Obadia Maregesi amesema ujenzi wa vyumba vinane vya madarasa
unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na miundombinu mingine muhimu itakamilika
kabla ya Septemba 2020.
Mbunge
wa jimbo, Profesa Muhongo ametoa wito kwa wazawa wa kata ya Nyamrandirira
wanaoishi nje ya kata hiyo kujitokeza kuchangia ujenzi wa shule hiyo.
(Habari na Hamisa Gamba,
Msaidizi wa Mbunge)
No comments:
Post a Comment