NEWS

Tuesday 28 April 2020

TRUMP: TUNACHOJUA KUHUSU HALI YA KIAFYA YA RAIS WA KOREA KASKAZINI KIM JOING UN


Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba anajua hali ya Kim Joing un , kufuatia madai kuhusu afya ya kiongozi huyo wa Korea Kaskzini.
Rais huyo alisema kwamba hawezi kutoa maelezo lakini anatumai kwamba bwana Kim yuko shwari.
Kumekuwa na uvumi uliokuwa ukizunguka tangu bwana Kim alipokosa kuhudhuria sherehe za kuadhimisha siku kuu muhimu.
Hatahivyo Maafisa wa Korea Kusini wanasema kwamba hakuna lisilo la kawaida nchini Korea Kaskazini.
Katika kikao cha faragha siku ya Jumapili waziri anayehusika na maswala ya kuleta amani kati ya mataifa hayo mawili Kim Yeon - chul alisema kwamba serikali ina uwezo wa kiintelijensia kusema kwamba hakuna kisicho cha kawaida kilichokuwa kikifanyika nchini humo.
Uvumi kuhusu hali ya kiafya ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ulianza baada ya kutoonekana katika maadhimisho ya sikukuu ilofanyika tarehe 15 mwezi Aprili.
Vyombo vya habari vya Korea Kusini wiki iliopita viliripoti kwamba Kim Joing un huenda alifanyiwa upasuaji wa moyo ama alikuwa amejitenga ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Hatahivyo pia vilisema kwamba ametuma ujumbe wa pongezi kwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga hoteli ya kitalii katika mji wa Wonsan , eneo ambalo vyombo vya habari vya Korea Kusini vinasema huenda ndiko Kim anakoishi.
'Msimamo wa serikali yetu ni thabiti'', Moon Chung-in, mshauri mkuu wa maswala ya kigeni wa rais wa Korea Kusini Moon Jae-in akijibu maoni ya vyombo vya habari nchini Marekani.
''Kim Jong un yuko hai na hali yake ni shwari. Amekuwa akiishi katika eneo la Wonsan tangu tarehe 13 mwerzi Aprili. Hakuna kisicho cha kawaida ambacho kimegunduliwa'', alisema akinukuliwa na chombo cha habari cha Aljazeera.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages