Watalaamu wa ubora wa
maji kutoka Ofisi ya Dakio la Mara Mori leo wamechukua sampuli za maji kutoka kwenye mgodi unaodaiwa kutiririsha
maji yenye kemikali ya sumu ambayo iliua ng’ombe 34 na kondoo mmoja katika kijiji cha Kewanja
jana April 27,2020 kwa ajili ya kufanyiwa uchungizi .
“ Mpango wa Dakio ni kutembelea na kukagua wachenjuaji wote wadogo
na wa kati ili kuona mioundo mbinu ya ,maji wanayotumia kama ni rafiki wa
mazingira”, Ofisa wa Dakio la Mara Mori
Mhandisi Mwita Mataro ameiambia Mara Online News mara baada ya
kukamilisha zoezi hilo.
Mhandisi Mwita amesema
mpango huwa utasaidia kuzuia madhara kama yalijitokeza jana pamoja na kulinda
vyanzo vya maji
safi
ReplyDelete