NEWS

Tuesday 28 April 2020

Hofu yatanda ukosefu wa maji Musoma



Wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wameingiwa hofu kwamba huenda wakashindwa kumudu kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona au COVID-19 baada ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) kutangaza kusimamisha usambazaji wa huduma ya maji kwa muda usiojulikana.

Wananchi hao wameeleza kustushwa na taarifa hiyo ya MUWASA hasa ikizingatiwa kuwa maji ndiyo silaha kubwa ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo, ambapo wataalamu wa afya na serikali wanahimiza watu kunawa mikona kwa sabuni na maji yanayotiririka mara kwa mara.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na ofisi ya Uhusiano MUWASA leo Jumatano Aprili 29, 2020, uzalishaji maji ya bomba umesimama kuanzia jana Jumanne Aprili 28, 2020 saa 12 jioni kutokana na hitilafu ya umeme katika kituo cha kuzalisha maji Bukanga.   

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages