RPC TarimeRorya William Mkonda |
Watu
wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Kisire lenye namba T 240
DST lililogongana na gari dogo lenye namba T 823 CWR aina ya Harrier, wilayani
Tarime, Mara.
Kamanda
wa Polisi Tarime Rorya, William Mkonda, amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na
kuwataja waliojeruhiwa kuwa ni dereva wa Harrier, Wanjabu Mgonja (38) na
abiria, Deogratius Makwizi (48).
Kamanda
Mkonda amesema ajali hiyo imetokea Aprili 20, 2020 saa 6:30 mchana katika
barabara ya Tarime – Mwanza kijijini Nyanjage.
“Majeruhi
wote wamefikishwa hospitali ya Mkoa wa Mara kwa matibabu,” amesema Kamanda Mkonda.
No comments:
Post a Comment