BENKI
ya CRDB imeahidi kuendesha huduma bora za kifedha kwa wanufaika 1,639 wa malipo
ya fidia kupisha mradi wa uchimbaji madini katika Mgodi wa Dhahabu wa North
Mara unaoendeshwa na kampuni ya Barrick katika eneo la Nyamongo wilayani
Tarime, mara.
Mkurugenzi
wa Wateja Wadogo wa Benki ya CRDB, Boma Raballa, ameyasema hayo leo Jumatano
Mei 20, 2020 mbele ya Waziri wa Madini, Dotto Biteko, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu na Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula katika hafla ya
uzinduzi wa malipo ya fidia hizo.
Aidha,
Raballa ameishukuru serikali kwa kuiamini CRDB na kuishirikisha kwenye mpango
huo, ambapo amesisitiza kuwa benki hiyo imejipanga kuhakikisha utekelezaji wake
unakidhi matarajio chanya ya pande zote.
“Ili
mpango huu wa ulipaji fidia uweze kufanikiwa, jambo kubwa ni kutoa elimu ya
kifedha kwa wananchi na kuweka mifumo madhubuti ya malipo kama vile miundombinu
ya huduma bora za kifedha,” amesema mkurugenzi huyo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula |
“Hivyo
sisi kama taasisi ya fedha, mkakati wetu wa kwanza tuliokuja nao ni kuanza
kutoa elimu ya matumizi bora ya fedha na tunaendesha kazi ya ufunguaji wa
akaunti kwa wakazi zaidi ya 2,000. Tunafanya kupitia tawi letu linalotembea
(mobile branch) ambalo litakuwa hapa,” amesema Raballa na kuongeza:
“Ufanikishaji
wa kazi hii ya ufunguaji wa akaunti utasaidia wananchi wote kupokea malipo yao
kwa uharaka katika njia usalama na kuepuka madhara yanayoweza kuambatana na
kukaa na fedha taslimu majumbani kwao, lakini pia wateja wote watakaofungua
akaunti wataunganishwa na huduma za simu benki na simu akauti ambazo
zitawawezesha kufanya miamala ya kifedha popote pale walipo.”
Raballa
ameongeza kuwa pamoaja na mkakati wa kutumia tawi linalotembea na CRDB Wakala,
benki hiyo tayari imefanya upembuzi yakinifu wa kufungua tawi rasmi mjini
Nyamongo na kwamba ujenzi huo utaanza na tawi hilo kufunguliwa rasmi ndani ya
mwezi mmoja kuanzia sasa.
“Tunatumaini
kuwa si tu tawi hilo litaongeza wigo wa upatikanaji huduma kwa wanufaika au
wakazi wa Nyamongo, bali litachochea na kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi
kupitia mikopo na huduma nyingine nyingi zinazotolewa na CRDB, hivyo niwasihi
Wananyamongo tukae mkao wa kula,” amesema Raballa.
No comments:
Post a Comment