NEWS

Sunday 24 May 2020

AICT YAWAKINGA WATOTO 150 DHIDI YA CORONA

Afisa Afya Wilaya ya Itilima, Oswin Mlelwa, akimkabidhi mmoja wa watoto vifaa vilivyotolewa na AICT.
KANISA la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Yeriko Inalo lililopo kata ya Luguru wilayani Itilima, Simiyu kupitia kituo chake cha Huduma kwa Mtoto, limetoa msaada wa vifaa kinga dhidi ya virusi vya corona kwa watoto 150 wanaoishi katika mazingira magumu.

Vifaa vilivyotolewa ni sabuni na ndoo maalumu za kunawia mikono vyenye gharama ya Sh milioni 2.2.
                    Baadhi ya vifaa vilivyotolewa

AICT imetoa vifaa hivyo kwa kushirikiano na washirika wenza ambao ni shirika la The Compassion lililopo jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo wilayani hapa Mei 23, 2020, Mratibu wa Kituo cha Huduma kwa Mtoto, Mary Steven, amesema wanalea watoto 150 na kuwawezesha kupata elimu ya makuzi na kiroho.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Inalo, Joseph Lubambe na Mchungaji wa Kanisa hilo, Elias Shitabo, wamesema  mara baada ya Rais Dkt John Magufuli kuwaondoa Watanzania hofu dhidi ya corona, wengi wamepata matumaini mapya, wanaishi bila hofu na kuendelea kuchapa kazi.

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Oswin Mlelwa, amewataka wananchi kuendeea kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na serikali juu ya tahadhari dhidi ya janga hilo.                (Habari  na Anita Balingilaki, Itilima)



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages