Mkurungenzi wa Kasedefo, Ezekiel Kasanga, akiongea wakati wa uzinduzi huo |
TAASISI ya Kawiye Social Development
Foundation (Kasodefo) yenye makao makuu wilayani Maswa, Simiyu imezindua
utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na janga la corona.
Mradi huo unalenga kuwafikia wakazi 60,000 wa wilaya hiyo iliyopo na hatimaye
kuiwezesha jamii kuwa na uelewa wa kutosha dhidi ya ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa Kasodefo, Ezekiel
Kasanga, amesema hivi karibuni kwamba mradi huo umegharimu Sh milioni
30,000,000 ambazo ni ruzuku inayotolewa na shirika la Foundation for Civil
Society (FCS).
Walengwa wa mradi huo ni wanawake, wazee na watoto, ambapo utekelezaji wake
unahusisha viongozi wa serikali ngazi ya wilaya, idara ya afya, wenyeviti wa
vijiji, viongozi wa dini, waganga wa tiba asili na wahudumu wa afya ngazi ya
jamii kwa kuzingatia mpango wa taifa wa kudhibiti ugonjwa huo. (Imeandikwa na Anita Balingilaki,
Itilima)
No comments:
Post a Comment