MBUNGE
wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ameanza kuchangia ujenzi wa wodi
za mama na mtoto katika zahanati za vijiji vya Bukima, Nyegina na Rukuba
Kisiwani.
Profesa
Sospeter Muhongo
Profesa
Muhongo ameiambia Mara Online News leo Mei 30, 2020 kwamba atachangia saruji
mifuko 600, kwa mchanganuo wa mifuko 200 kwa kila zahanati, itakayotolewa
kulingana na kasi ya ujenzi.
Mbunge
huyo anatoa mchango huo kuunga mkono juhudi za wakazi wa vijiji hivyo na
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini katika ujenzi wa wodi hizo kwa ajili
ya kuboresha huduma za mama na mtoto.
(Imeandikwa na
Mara Online News)
No comments:
Post a Comment