NEWS

Tuesday 26 May 2020

Sababu za Soi kuomba Udhamini CWT Taifa


MWALIMU Francis Soi mwenye elimu ya Shahada ya Pili ya Elimu, Uongozi na Sera (China), ametaja sababu za yeye kuomba nafasi ya Udhamini wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Taifa kuwa ni kutaka kushirikiana na viongozi wengine katika kuimarisha uhai na ustawi endelevu wa chama hicho.

Katika mazungumzo yake na Mara Online News leo Mei 26, 2020, Soi ametaja sababu nyingine kuwa ni kufanya tathmini ya usalama wa mali za CWT, kutatua changamoto za utumishi na umiliki wa mali za chama, kuwezesha utekelezaji wa mipango mikakati, kustawisha utekelezaji wa sera, kuwezesha mabadiliko ya kisasa katika utambuzi na uhifadhi wa mali za chama hicho.
Mwalimu Francis Soi
Amesema ametaja njia atakazotumia kutekeleza hayo kuwa ni pamoja na majadiliano yanayohusisha vikao vya kikatiba, ufuatiliaji, uandaaji mipango ya muda mfupi na mrefu, mafunzo ya kisheria kwa viongozi wa wilaya na mikoa, ushirikiano na ushawishi wa pamoja.

Mwalimu Soi amesema ana uzoefu katika uongozi kwani amekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CWT Wilaya mwaka 2020, Mjumbe wa Mkutano Mkuu (2015-2020) na Kiongozi wa Wilaya (2010-2015).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages