MWALIMU
Francis Soi mwenye elimu ya Shahada ya Pili ya Elimu, Uongozi na Sera (China),
ametaja sababu za yeye kuomba nafasi ya Udhamini wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT) Taifa kuwa ni kutaka kushirikiana na viongozi wengine katika kuimarisha
uhai na ustawi endelevu wa chama hicho.
Katika
mazungumzo yake na Mara Online News leo Mei 26, 2020, Soi ametaja sababu
nyingine kuwa ni kufanya tathmini ya usalama wa mali za CWT, kutatua changamoto
za utumishi na umiliki wa mali za chama, kuwezesha utekelezaji wa mipango
mikakati, kustawisha utekelezaji wa sera, kuwezesha mabadiliko ya kisasa katika
utambuzi na uhifadhi wa mali za chama hicho.
Mwalimu Francis Soi |
Amesema
ametaja njia atakazotumia kutekeleza hayo kuwa ni pamoja na majadiliano
yanayohusisha vikao vya kikatiba, ufuatiliaji, uandaaji mipango ya muda mfupi
na mrefu, mafunzo ya kisheria kwa viongozi wa wilaya na mikoa, ushirikiano na
ushawishi wa pamoja.
Mwalimu
Soi amesema ana uzoefu katika uongozi kwani amekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya
CWT Wilaya mwaka 2020, Mjumbe wa Mkutano Mkuu (2015-2020) na Kiongozi wa Wilaya
(2010-2015).
No comments:
Post a Comment