Katika
hotuba yake wakati wa ziara hiyo leo asubuhi Mei 26, 2020, Naibu Waziri Waitara
amesema kitendo cha kutumia jina la Mara kwenye vyombo hivyo vya habari
kinamuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alizaliwa
katika mkoa wa Mara.
Mhariri
wa Habari, Christopher Gamaina (kulia) akimwonesha Naibu Waziri Waitara (hayupo
pichani) Gazeti la Sauti ya Mara
|
Waitara
ametumia nafasi hiyo pia kumpongeza Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya
Mara Online inayomiliki vyombo hivyo vya habari, Mugini Jacob kwa ubunifu wa
kuvianzisha na kutoa ajira kwa vijana kadhaa na kwa kuzingatia usawa wa
kijinsia.
Amepongeza
pia kaulimbiu ya Gazeti ya Sauti ya Mara inayosema “Habari kwa Maendeleo”
akisema inachochea uandishi wa habari za maendeleo ya wananchi yakiwamo
yanayowezeshwa na serikali.
Add caption |
Mkuu wa kitengo cha graphics Mara online Rajabu Mpella
akimueleza Naibu Waziri wa TAMISEMI kuhusu
uandaaji wa gazeti la Sauti ya Mara
Aidha,
ameeleza kuvutiwa na habari zinazochapishwa na Sauti ya Mara na kuwaomba
waandishi wa gazeti hilo kuendelea na sera hiyo kwa kuzingatia maadili ya
taaluma ya habari.
Naye Mlezi wa Gazeti la Sauti ya Mara, Simon Mseti, amemweleza Naibu Waziri huyo kwamba anaridhishwa na mwenendo wa gazeti hilo katika kuhamasisha maendeleo ya mkoa wa Mara, Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa jumla.
Naibu Waziri Waitara akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za Mara Online
Kwa
upande wake, CEO wa Mara Online, Jacob, amemshukuru Naibu Waziri Waitara kwa
ziara hiyo na kuahidi kuzingatia ushauri wake kuhusu kuelekeza nguvu kubwa pia katika
kuandika habari za kuelimisha wananchi juu ya kuepuka migogoro ya ardhi na mila
zilizopitwa na wakati ikiwemo ya ukeketaji.
Naibu
Waziri, Mwita Waitara (wa nne waliosimama nyuma) katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Sauti ya Mara
|
Gazeti
la Sauti ya Mara lilizinduliwa Januari 13, 2020 na Mkuu wa Wilaya ya Tarime,
Mhandisi Mtemi Msafiri kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
(Imeandikwa na
Mara Online News, Tarime)
No comments:
Post a Comment