NEWS

Tuesday 5 May 2020

Sherehe za mavuno marufuku Bariadi


Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga (katikati) akipokea vifaa kinga binafsi kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni ya mafuta ya Nengelo Heri Mchunga iliyopo mjini Bariadi.

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amepiga marufuku sherehe za mavuno (mbina ) lengo likiwa kupunguza misongamano ili  jamii iweze kujinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa vifaa kinga binafsi (Personal Protective Equipment  _PPE) na kifaa cha kupimia joto la mwili kutoka kwenye kampuni ya mafuta ya Nengelo iliyopo mjini Bariadi.

Sherehe  hizo (mbina ) ufanyika kila mwaka kwaajili ya kusherekea mavuno  na ujumuisha idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali.

" sherehe za mbina marufuku mpaka hapo hali itakapokuwa nzuri ...kama mjuavyo sherehe hizi ukutanisha idadi kubwa ya watu kutoka maeneo tofauti tofauti msongamano unakuwa mkubwa mimi niwatake wananchi kufuata taratibu zote zinazotolewa na wizara ya afya "alisema Kiswaga na kuongeza kuwa:

"niwatake jeshi la polisi kuwakamata wale wote watakaokiuka maelekezo haya" aliongeza  Kiswaga

Pamoja na hayo awali akipokea msaada huo Kiswaga amesema  umekuja wakati muafaka ambapo utawasaidia watoa huduma kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Akikabidhi vifaa hivyo mkurugenzi wa kampuni ya hiyo Heri Mchunga amesema wametoa vifaa hivyo kwaajili ya watoa huduma za kiafya  wakiwemo madaktari ,wauguzi na manesi ili akitokea mtu mwenye dalili za ugonjwa huo waweze kujikinga kuambukizwa na kuwaambukiza wengine.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga (katikati) akionesha kifaa cha kupimia joto kilichotolewa na kampuni ya mafuta ya Nengelo iliyopo mjini Bariadi.


Aidha ameongeza kuwa vifaa hivyo ni vifaa kinga binafsi (Personal Protective Equipment  _ PPE) 7 na kifaa cha kupimia joto kimoja ambacho amekikabidhi kwenye kituo cha polisi Bariadi vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja.

Wakiongea kwa niaba ya watumishi wa afya  wa wilaya ya Bariadi Dkt Judith Ringia ambaye ni mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Bariadi na Dkt Joseph Mziba ambaye ni  mganga mkuu wa wilaya ya Bariadi wamesema vifaa hivyo vitawakinga watumishi wa afya wakati wakutekeleza majukumu yao hususan kipindi hiki cha kukabiliana na janga la corona  na hivyo kufanya kazi bila hofu ya kuogopa kupata maambukizi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo.

Aidha kwa upande wake mkuu we jeshi la polisi wilaya ya Bariadi (OCD) Hussa Anderson Mwaikombo ambaye amepokea kifaa cha kupimia joto la mwili kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu amesema jeshi la polisi ni miongoni mwa taasisi zinazopokea watu wengi wakiwemo watuhumiwa na mashahidi hivyo kifaa hicho kitawasaidia kuwapima wale wote wanaoingia kituoni hapo wakiwemo watumishi wa kituo hicho.

Katika hatua nyingine Kiswaga amesema kuwa fedha zilizochangwa na wadau April 28, 2020 zimetumia kununulia vifaa kinga binafsi (PPE)  10 ambazo zina uwezo wa kusafishwa vizuri baaada ya matumizi na kutumika tena na  leo zimekabidhiwa kwa waganga wakuu wa halmashauri ya mji na wilaya na hivyo kufanya jumla ya vifaa kinga hivyo (PPE) kufikia 17.(Habari na Anita Balingiliaki Bariadi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages