NEWS

Monday 4 May 2020

RC MTAKA AZINDUA MPANGO WA MASOMO KWA NJIA YA MTANDAO KWA WANAFUNZI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka


Katika kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na janga la Corona Mkoa wa Simiyu umezindua mpango mkakati wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kusoma kwa njia ya mtandao kwenye kipindi hiki cha likizo ya  dharula ili kujikinga na ugonjwa   wa homa ya mapafu( covid 19).

Mkakati huo umezinduliwa leo kwenye  shule ya  sekondari Simiyu  iliyopo mjini Bariadi na mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka .

Mtaka amesema kuwa mkakati huo utawasaidia wanafunzi kupata masomo wakiwa nyumbani kutoka kwa walimu wao huku ukiwa na malengo makuu manne ambayo yataufanya mkoa kuendelea kufanya vizuri kitaifa kama ilivyo adhima ya kushika nafasi ya tatu bora kitaifa.

" malengo makuu ya mkakati huo ni kumwezesha mwanafunzi kuendelea kujifunza,walimu kuwa na mawasiliano ya kitaaluma kwa wanafunzi  wao,wazazi kufanya ufuatiliaji wa taaluma kwa watoto wao pamoja na watoto kutulia nyumbani wakijisomea kipindi hiki cha likizo ya dharula"alisema Mtaka 

Pamoja na hayo amewataka wazazi /walezi kuwahimiza wanafunzi  kujisomea kupitia vipindi vinavyorushwa kupitia channel  mbalimbali nchini na si muda wa vipindi kurushwa watoto wanapewa shughuli mbalimbali ikiwemo za kufanya biashara mitaani.

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Bariadi Andrew Chenge  ametoa msaada wa kompyuta 5 na mashine ya kudurufu kutoka mamlaka ya mawasiliano kwa wote ambazo zimekabidhiwa kwa mkuu wa mkoa huo na Christina Chenge (mke wa mbunge huyo) kwa niaba ya mbunge.


 Chenge amesema kuwa kompyuta hizo zitumike kwa kazi na malengo yaliyokusudiwa ili mkoa wa Simiyu uzidi kuwa kileleni.

Akiongea mara baada ya makabidhiano ya komputa na mashine ya kudurufu mkuu we wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amesema kuwa hategemei shule hiyo (Simiyu sekondari) iliyokabidhiwa vifaa hivyo kupata wanafunzi wenye daraja sifuri kwani tayari wana walimu  na vifaa vya kutosha sambamba na madarasa ya kutosha.

Nae mkuu wa shule ya Simiyu Sekondari Paul Susu amemshukuru mhe Chenge kwa kutambua uhitaji wa kompyuta walionao kwani utawasaidia katika kutekeleza shughuli zao za ufundishaji huku akiongeza kuwa pamoja na kuwa shule ya Simiyu ndio imekabidhiwa lakini zitasaidia shule nyingi kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano na shule zingine mkoani hapo.


Nao baadhi ya walimu wa shule hiyo akiwemo Dorine Bella na John Mogela wamesema kuwa ujio wa  kompyuta hizo utakuwa chachu ya kurahisisha ufundishaji kipindi hiki cha ugonjwa wa homa ya mapafu na baada ya ugonjwa huo.

Mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa mpango mkakati na makabidhiano Mtaka aliongoza zoezi la ukaguzi wa maedeleo ya ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Simiyu.


(Habari Na Anita Balingiliaki,Bariadi.)


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages