Kamanda
Muliro Jumanne Muliro
|
POLISI
mkoani Mwanza wamewakamata watuhumiwa wawili wa mauaji ya Ndebeto Kakula mwenye
umri wa miaka 78, mkazi wa kijiji cha Mwankali wilayani Misungwi, Mwanza.
Taarifa
ya Kamanda wa Polisi Mwanza, Muliro Jumanne Muliro kwa waandishi wa habari leo
Mei 4, 2020 imewataja wanaoshikiliwa kwa mauaji hayo kuwa ni Rodha Shabani (27)
na Muhangwa Paul, wakazi wa kijiji cha Mwankali.
Kwa
mujibu wa Kamanda Muliro, Shabani amehojiwa na kukiri kumuua mzee huyo kwa
kumkata na panga shingoni wakati akitoka kuteka maji kisimani kijijini hapo,
Aprili 29, 2020, saa 2:20 asubuhi.
Kamanda
huyo amefafanua kuwa Shabani alitenda mauaji hayo baada ya Paul ambaye ni mganga
wa kienyeji kumpigia ramli na kumwambia kwamba mzee huyo ndiye aliwaroga watoto
wake wawili na kusababisha vifo vyao.
“Upelelezi
wa shauri hili umekamilika kwa asilimia 90 na watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani haraka iwezekanavyo,” amesema Kamanda Muliro.
(Habari na
Christopher Gamaina, Mwanza)
No comments:
Post a Comment