NEWS

Monday 1 June 2020

REO ashiriki mapokezi Kidato cha 6 Tarime sekondari

Afisa Elimu Mkoa wa Mara (REO)  Ephraim Simbeye leo Juni 1, 2020 ameshiriki katika mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Tarime.

Afisa Elimu Mkoa wa Mara Ephraim Simbeye (Watatu kulia) akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa kidato cha sita jinsi ya kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kusoma kwa bidii
 Simbeye ameridhishwa na maandalizi yaliyofaywa na uongozi wa shule ya Tarime sekondari katika kupokea wanafunzi hao hususani hatua za kuwakinga na tatizo la COVID-19.
Mkuu wa shule ya Sekondari Tarime  Machota Kora akimpokea afisa elimu mkoa wa Mara  Ephraim Simbeye alipotembelea shuleni hapo
  Alitumia fursa hiyo kuwataka walimu wa shule zote zenye kidato cha sita kuhakikisha wanafunzi hao wanasoma kwa bidii ili kufanya  vizuri katika mtihani ulio mbele yao huku akisisitiza kuwa divisini zero haikubaliki hivi sasa katika mkoa huo.

Walimu tufanyeni kazi kwa kujituma niliwahi kusoma mahala fulani kuwa ualimu ni wito hivyo wito huo uonekane katika ufaulu hatutaki alama ‘zero’alisisitiza REO Simbeye.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wakinawa mikono kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona

Kwa upande wake  Mkuu wa Shule ya Sekondari Tarime, Machota Kora amemhakikishia REO huyo kuwa wameandaa utaratibu mzuri kuwanoa wanafunzi hao ili waweze kufanya vizuri katika mtihani wao.

“ Tayari tumemaliza  mada zote hivyo tunachofanya kwa sasa ni kufanya marudio na nitahakikisha nakuwepo pamoja na walimu wangu wakati wa muda wa usiku wa kujisomea kwa wanafunzi hao ili kuhakikisha tunatoa msaada pale wanafunzi hao watakapokwama’’ alisema Machota.
Wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa paredi
Welenfrid Shangwe  ambaye ni mwalimu wa taaluma katika shule hiyo amesema wameweka mikakati mbalimbali ikiwemo kufanya maadalizi ya jioni  yatakayohusisha walimu na wanafunzi kushiriki katika kujadili na kufanya mazoezi katika masomo. 

(Habari na Clonel Mwegendao, Tarime)



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages