NEWS

Saturday 30 May 2020

Waitara ahudhuria mazishi mzazi wa PKM, ahimiza amani

 NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara, leo Mei 30,2020 ameungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Aneth Batholomeo ambaye ni mama mzazi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya PKM, Pastory Batholomeo Machage.
Naibu Waziri Waitara (wa pili kulia) na wananchi wengine katika mazishi hayo

 Mazishi hayo yamefanyika nyumbani kwa marehemu Nyamongo na kuhudhuriwa na wananchi, viongozi wa serikali na vyama vya sisasa na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Akiongea katika mazishi hayo, Naibu Waziri Waitara ametoa pole kwa familia ya Batholomeo Machage kwa kuondokewa na mama yao.
Naibu Waziri Waitara akitoa salamu za pole kwa familia


Waitara ametumia nafasi hiyo pia kuonya kuwa serikali haitawavumilia wanasiasa wanaochochea migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo wilayani Tarime.

Amesema uchochezi huo unaweza kusabbisha uvunjifu wa amani ambayo hivi sasa imetamalaki wilayani humo.
Wakili Otieno Onyango (katikati mwenye miwani) akiwa na baadhi ya wananchi wa Nyamongo

“Mimi kama mwenyeji wa Tarime, kijana wenu na ambaye nimebahatika kuwa katika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli, tunajua kumekuwepo na malalamiko miaka ya nyuma ya ulipwaji wa fidia hapa Nyamongo, lakini Awamu ya Tano imeanza kusimamia ulipwaji wa fidia hizo na hili katika ustaarabu wa kawaida ni jambo la kumshukuru Rais Magufuli,” amesema Waitara.
Naibu Waziri Waitara akisaini kitabu cha rambirambi


Naibu Waziri huyo wa Tamisemi amewataka wananchi kupokea malipo hayo na kuwaomba wenye malalamiko watumie njia sahihi kuyafikisha serikalini.
Mkurugenzi wa kampuni ya PKM Pastory Batholomeo Machage (wapili kutoka kulia) akipokea rambirambi kutoka kwa wanachama wenzake wa kikundi cha Nyamongo Saving Group. Wakwanza kushoto  ni kada wa CCM Nicodemus Keraryo


(Imeandikwa na Clonel Mwegendao, Nyamongo)

1 comment:

  1. Habar za sauti ya Mara ni Moto hongeren sana kwa kazi nzur mnazozifanya mbarikiwe sana

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages