NEWS

Wednesday 29 July 2020

Choo chaua wanafunzi wawili Rorya


WANAFUNZI wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa choo jana Julai 28, 2020 katika Shule ya Sekondari ya Ngasaro wilayani Rorya, Mara. Kufuatia maafa hayo, viongozi wameanzisha harambee ya dharura na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 1.185 kwa ajili ya kugharimia ujenzi wa choo kipya shuleni hapo.
Pichani: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye (aliyevaa kofia nyeusi) na Mbunge wa Rorya  anayemaliza muda wake Lameck Airo (aliyevaa suti) na wananchi wengine wakiangalia ukuta wa choo ulioanguka na kusababisha vifo vya wanafunzi wawili na kujeruhi mmoja shuleni hapo.( Habari, Picha na Clonel Mwegandao)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages