NEWS

Friday 17 July 2020

Makada 468 CCM wanyukana ubunge mkoani Mara

Ngatiche

WANACHAMA 468 wa CCM wakiwamo wanaume 434 na wanawake 34 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge katika majimbo 10 ya uchaguzi yanayounda mkoa wa Mara, huku 10 kati yao wakishindwa kurejesha fomu zao hadi pazia la shughuli hiyo linafungwa jana Julai 17, 2020.

Majimbo yanayounda mkoa wa Mara ni Musoma Mjini, Musoma Vijijini, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Serengeti, Rorya, Butiama, Bunda Mjini, Bunda Vijijini na Mwibara.

Kanali mstaafu Kichonge Mahende, mwania ubunge Tarime Mjini

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mkoa wa Mara kama si Tanzania, Jimbo la Bunda Mjini limeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi ya ubunge.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Shaibu Ngatiche, ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu jana jioni kuwa makada wa chama hicho waliochukua na kurejesha fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Bunda Mjini ni 74, wakifuatiwa na Jimbo la Musoma Mjini (64).


                                              Stephen Wasira(kushoto), mwania ubunge Bunda Mjini

Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha ubunge Jimbo la Bunda Mjini ni kada mkongwe wa CCM na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Stephen Wasira (pichani kushoto).

Ngatiche ametaja majimbo mengine na idadi ya waliochukua fomu za kuwania ubunge ikiwa kwenye mabano kuwa ni Serengeti (59), Butiama (59), Rorya (52), Mwibara (40), Musoma Vijijini (35), Bunda Vijijini (31), Tarime Vijijini (30) na Tarime Mjini (25).
 
Sophia Bhoke Maryogo, mwania ubunge Musoma Mjini
Aidha, Ngatiche amesema wanawake 44 walijitokeza kuchukua fomu za kuwania Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara kupitia Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), 13 kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na mmoja kupitia Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages