Viongozi wa TCRA, UTPC na MPC katika hafla ya uzinduzi wa blogu ya Mwanza Press Club |
KLABU
ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MZA) leo Jumatatu Julai 20, 2020
imezidua blogu yake inayoitwa Mwanza Press Club kwa ajili ya kutumiwa
na wanachama wa klabu hiyo kuandika habari na makala mbalimbali za ndani
na nje ya mkoa huo.
Mgeni
rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza
amekuwa Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa,
Mhandisi Francis Mihayo, ambapo pia Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan na Mwenyekiti wa
MPC, Edwin Soko, walihudburia.#Mara Online News
No comments:
Post a Comment